Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais aliewekwa kizuizini na Wanajeshi ajiuzulu

54616872 303 660x394 Rais aliewekwa kizuizini na Wanajeshi ajiuzulu

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametangaza kujiuzulu kupitia televisheni, saa chache baada ya wanajeshi waasi kumkamata sambamba na Waziri wake mkuu Boubou Cisse katika mji mkuu wa Bamako.

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametangaza kujiuzulu kupitia televisheni, saa chache baada ya wanajeshi waasi kumkamata sambamba na Waziri wake mkuu Boubou Cisse katika mji mkuu wa Bamako.  Akizungumza kupitia kituo cha utangazaji cha taifa ORTM, Keita amesema kuwa kujiuzulu kwake kunaanza mara moja. Awali picha na vidio zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha msafara unaoaminika kuwa wa rais Keita na waziri mkuu Cisse uliokuwa umezingirwa na wanajeshi.Kukamatwa kwa viongozi hao kuna litumbukiza taifa hilo ambalo tayari linakabiliwa na makundi ya wanajihadi na maandamano katika mgogoro mkubwa.Picha na vidio zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha msafara unaoaminika kuwa wa rais Keita na waziri mkuu Cisse uliokuwa umezingirwa na wanajeshi, waliokuwa wakitembea bila woga kwenye mitaa ya Bamako.Kiongozi mmoja wa waasi aliyezungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina amesema kuwa “rais na waziri mkuu wako chini ya udhibiti wetu, baada ya kukamatwa katika makazi ya Keita mjini Bamako”Afisa mmoja wa jeshi Sidi Gakao amethibitisha taarifa hizo alipozungumza na shirika la habari la DPA kwa njia ya simu akisema kwamba “rais na waziri wake mkuu wamekamatwa”.Wanajeshi walianza uasi huo mapema siku ya Jumanne katika mji wa Kati, uliopo kilometa 15 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Bamako ambapo milio ya risasi ilisikika. Taarifa za kukamatwa viongozi wa serikali zilipokelewa kwa furaha na umati wa watu waliokuwa wamekusanyika katikati ya mji kwa ajili ya kushinikiza Keita kujizulu.BIBI MZEE AELEZA ALIVYOWAHUDUMIA WAKINA NYERERE, KAWAWA, “NILIKUWA MZURI, NIMEKULA NAO MIHOGO”

Chanzo: millardayo.com