Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Zambia kujulikana ndani ya saa 72

ZAMBIA12 Uchaguzi Mkuu Zambia

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni siku moja tangu wananchi nchini Zambia watimize haki yao ya Kikatiba ya kupiga kura kwa nafasi ya Rais, zoezi la la kuhesabu kura linaendelea nchi humo.

Tume ya Taifa ya uchaguzi, imethibitisha kuanza kwa zoezi hilo na kusema kuwa matokeo kamili yatatangazwa baada ya saa 72 tangu zoezi la upigaji kura kumalizika.

Katika uchaguzi huu, Rais aliyepo madarakani, Edgar Lungu, anachuana vikali na mpinzani wake Haikande Hichilema, kwa hoja moto huku kila mmoja akijinasibu kwa sera ya uchumi.

Hata hivyo vijana wanatajwa kuwa sehemu kubwa ya Uchaguzi huo, kwa kushiriki kwa asilimia kubwa, hali inayoonesha utayari wao katika kuleta mabadiliko kwa taifa lao hususiani ni Uchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live