Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Yahya Jammeh kushtakiwa

Yahya Jammeh Yahya Jammeh

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Sheria ya Marekani imesema imefanikiwa kutaifisha jumba la kifahari lililonunuliwa na Rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh kwa dola milioni 3.5 kwa madai kwamba lilinunuliwa kwa pesa za rushwa.

Jumba hilo lililopo Potomac, Maryland limechukuliwa na Marekani pamoja na mapato yote ya kukodisha yanayotokana na mali hiyo tangu malalamiko yalipowasilishwa mwaka 2020.

Marekani imesema inakusudia kuuza mali hiyo na imependekeza kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba mapato yatokanayo na mauzo ya mali hiyo yatumike kuwanufaisha Watu wa Gambia walioumizwa na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ya Rais huyo wa zamani.

Rais huyo wa zamani anashutumiwa kwa kula njama na familia yake na Washirika wake kwa kutumia makampuni ya nje ya Nchi na amana za nje ya Nchi kujipa mapato yake yanayodaiwa kuwa ya kifisadi ambapo Serikali ya Gambia wiki hii ilisema iko tayari kumfungulia mashitaka kwa kile ilichokiita mamia ya uhalifu alioufanya wakati wa utawala wake. #TanzaniaWeb.Com

Chanzo: www.tanzaniaweb.live