Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais William Ruto awataka madaktari kusitisha mgomo wao na kurejea kazini

Rais William Ruto Awataka Madaktari Kusitisha Mgomo Wao Na Kurejea Kazini Rais William Ruto awataka madaktari kusitisha mgomo wao na kurejea kazini

Wed, 1 May 2024 Chanzo: Bbc

Rais William Ruto amewataka madaktari kusitisha mgomo wao huku serikali ikijitahidi kutimiza matakwa yao yote katika wakati ambao haujabainishwa siku zijazo.

Katika hotuba yake ya Siku ya Wafanyakazi kwenye bustani ya Uhuru Gardens jijini Nairobi, Ruto aliwaambia madaktari kuwa serikali haiwezi kutimiza matakwa yao yote kikamilifu kutokana na matatizo ya kifedha.

“Tumewasilisha kile ambacho serikali iko tayari kufanya; 17 kati ya madai 19, mengine hayawezekani kwa sababu ya matatizo ya kifedha,” alisema.

“Nawaomba madaktari warudi kazini, tutasuluhisha, turekebishe uchumi na kila mtu atapata haki yake siku za usoni. Lazima tuwe waaminifu kwa kila mmoja hata kama inauma, hakuna haja ya kusema uwongo."

Tangu Machi 14, madaktari wamekuwa wakigoma na kupinga hatua ya serikali kushindwa kuwapa kazi madaktari tarajali na kutekeleza Mkataba wa Majadiliano ya Pamoja (CBA) wa 2017 kuhusu masharti ya kazi ya madaktari.

Huku mgomo huo ukiingia siku ya 49 hii leo, Rais Ruto, aliwataka madaktari kuzingatia athari za mgomo wao katika huduma za afya nchini na kurejelea majukumu yao kwa kile alichotaja kuwa ustawi wa umma.

Chanzo: Bbc