Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru kuzuru ngome ya Ruto huku tofauti zao zikishamiri

93900433c0505e72 Rais Uhuru kuzuru ngome ya Ruto huku tofauti zao zikishamiri

Wed, 23 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Rais atatua kaunti za Trans Nzoia, Uasin Gishu na Nakuru kukagua miradi ya serikali yake

- Wadadisi wanasubiri kuona hali itakavyokuwa kwani kaunti hizo ni baadhi ya ngome za DP kisiasa

- Wandani wa DP wamekuwa wakilia kuhusu anachopitia DP serikalini licha ya wao kumuunga mkono Rais

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzuru ngome ya kisiasa ya naibu wake William Ruto ya Bonde la Ufa.

Ziara hiyo ya maendeleo inajiri wakati ambapo wawili hao wameweka wazi kuwa ndoa yao imepasuka kiasi cha kurushiana cheche za maneno hadharani.

Kwa mujibu wa duru za kuaminika, Rais atakuwa maeneo ya Trans Nzoia, Uasin Gishu na Nakuru kukagua miradi ya maendeleo inayoendeshwa na serikali yake.

Bonde la Ufa ni ngome ya Ruto ambapo huwa na wafuasi sugu na wamekuwa wakilalamika kuwa wamesalitiwa na Rais.



Mkataba wa kisiasa kati ya Rais na Raila Odinga wa handisheki ulimuweka Ruto nje ya serikali kiasi cha kumfanya kulia kwenye vyombo vya habari.

Wafuasi wake wamekuwa wakilaumu Rais kwa kumtema DP wakisema sasa ameungana na waliokuwa wapinzani wao 2013 na 2017.

Aidha tayari kuwa duru kuwa Rais anapanga kuunga mkono muungano wa NASA kwenye siasa za 2022.



Wadadisi wa siasa wanasubiri kuona ni nani atampokea Rais katika eneo hilo ambapo kwa kawaida Ruto amekuwa akimkaribisha.

Tayari Ruto amesema hadharani kuwa hana haja na chama cha Rais za Jubilee kwenye uchaguzi ujao akisema amejipanga.

Wamekwama na chama yote, sasa wanataka kunganisha ODM na Jubilee, sasa historia ya Kenya jamani sijui itakuwaje,….wanafikiria hustler tutakosa chama ya kutupeleka mbele, tuko macho, tuko na chama ya mahusstler , inaitwa UDA,” alidokeza.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke