Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru kufanya sherehe ya mwisho Jamhuri Uhuru Park

0466964d0a1a2325 Rais Uhuru kufanya sherehe ya mwisho Jamhuri Uhuru Park

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

RaisKenyatta anatarajia kuwahutubia Wakenya kwa hotuba ya mwisho. Wakenya 11, 000 pekee ndio wataruhusiwa katika bustani ya Uhuru kuhudhuria sherehe za Jamhuri Dei Disemba 13.

Sherehe za Jamhuri zitafanyika Jumatatu Disemba 13 katika bustani ya Uhuru ambapo Wakenya 11, 000 pekee watahudhuriaItakuwa ni sherehe ya Jamhuri ya mwisho kwa rais Uhuru kwani mwaka ujao Ikulu itakuwa na mwenyeweWakenya wanasubiri kuskia ujumbe ambao

Sherehe hizo huwa kila Disemba 12 lakini inapokuwa siku ya Jumapili hupelekwa Jumatatu kama ilivyo mwaka huu.

Sherehe hizo huwa za kufurahia siku ambayo Kenya ilipata uhuru wa kujitawala kutoka kwa wakoloni.

Katibu katika wizara ya Usalama wa Ndani Karanja Kibicho alisema ni Wakenya wachache tu wataruhusiwa kuingia bustani ya Uhuru kwa mujibu wa sheria za Covid-19.

"Kwa mujibu wa sheria za kukabili Covid-19, tutaruhusu watu 10, 000 pekee katika eneo la kuketii na watu wengine 1, 000 katika jukwaa ya wageni. Wanaotarajiwa kufika watapokea mwaliko kupitia Nyumba Kumi na maafisa wengine wa serikali ili kuhakikisha kuwa kila watu wanaakilishwa ipasavyo," katibu Kibicho alisema

Ukarabati umekuwa ukifanywa katika bustani hiyo tayari kwa maadhimisho hayo ambapo wageni tajika hualikwa.

Kibicho alisema serikali itafanya maamuzi iwapo sherehe hizo pia zitafanyika katika kaunti kama ilivyokuwa hapo awali.

"Tangu mlipuko wa janga la Covid-19 nchini, tumekuwa tukifanya sherehe moja ya kitaifa ambayo huongozwa na Rais huku wengine wakifuatilia kwenye runinga. Bado hatujakabili janga hili. Uamuzi wa iwapo kutakuwa na sherehe katika kaunti utafanywa hii wikendi," Kibicho aliongeza.

Sherehe hiyo itakuwa ya mwisho kwa Rais Uhuru Kenyatta kwani mwaka ujao uchaguzi mkuu utafanyika na kiongozi mpya kuchukua hatamu katika Ikulu.

Wakenya watakuwa wametege maskio ili kupata ujumbe wa mwisho kwa Rais katika sherehe za Mashujaa.

Amekuwa akitumia nafasi kama hiyo kuwapa Wakenya hisia sana kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke