Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru azawadi mama aliyekutana naye msiitu wa Gakoe Kieni

2e045a258b6701ca Rais Uhuru azawadi mama aliyekutana naye msiitu wa Gakoe Kieni

Fri, 23 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wanjiku alisema ilikuwa furaha kubwa kukutana na Rais Uhuru katika mradi wa maji wa Gakoe Gatundu KaskaziniWalikutana alipompata Rais akijaribu kufungua lango na akamsaidia bila kujua ni rasmiWakati huo hawakuweza kusemezana naye kwa kirefu kwani alikuwa na haraka ya kuondokaBaadaye walizungumza na runinga na kutuma ombi lao ambalo Uhuru ametimiza mara mojaRais Uhuru Kenyatta ametimiza ndoto ya mama aliyekutana naye katika msitu wa Kieni Gatundu Kaskazini alipokuwa ameenda kukagua mradi wa maji.

Eunice Wanjiku na wanawe wawili walikuwa kwenye zoezi la kutafuta kuni walipokutana na Rais.

Kulingana na simulizi walizotoa kwa runinga ya Inooro baadaye, walikuwa katika msitu wa Kieni kutafuta kuni wakati walikutana na 'mzee aliyeomba usaidizi wao'.

Bila kujua alikuwa ni Rais, 'mzee' huyo aliomba wamsaidie kufungua lango la mradi wa maji wa Kieni na wakafanya hivyo huku wakimuonya kuwa huenda akajipata pabaya maafisa wa eneo hilo wakimuangukia.



Read also

NIS Ilionya Rais Uhuru Kwamba Jubilee Itabwagwa na UDA Kiambaa



Ni wakati wa kufungua lango ambapo maski ya Rais ilianguka na mwanawe Wanjiku akamtambua na kumjulisha mamake kuwa alikuwa na kiongozi wa taifa.

Alishtuka na licha ya kupata muda wa kupiga picha, hakupata nafasi ya kumwambia Rais chochote kwani Uhuru alikuwa na haraka ya kuondoka.

Akiongea na runinga hiyo, alisema iwapo angekuwa na nafasi angemuomba Rais kumnunulia ng'ombe ili ajikimu kimaisha.



Rais alitii ombi la mama huyo na kumpa ng'ombe wawili waliofikishwa nyumbani kwao Gakoe.

Wanjiku alisema alikuwa ameshtuka wakati huo kwani walishtuka sana kukutana na kiongozi wa taifa.

"Sikuweze kupata nafasi ya kumwambia lolote, lakini kwa sasa ningemwambia kweli aninunulie ng'ombe ili niwezage kujikimu pamoja na huyu msichana wangu," alisema Wanjiku.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke



Read also

Kangogo Alisafiri Mombasa Kumuua Aliyekuwa Mumewe Lakini Akamsamehe
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke