Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru awarai Wakenya kupasisha BBI ili wanufaike na matunda yake

5919bf0ee332300c Rais Uhuru awarai Wakenya kupasisha BBI ili wanufaike na matunda yake

Fri, 23 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta alipigia debe BBI na kusema kwamba Wakenya watakuwa na fursa ya kufurahia haki na uhuru waoUhuru aliyasema haya wakati mchakato wa BBI unazidi kukumbwa na hali ya sintofahamuHii ni baada ya Mahakama kuu kuufutilia mbali mchakato huo mzimaRais Uhuru Kenyatta amewataka Wakenya kuupasisha Mchakayo wa Maridhiano (BBI) jinsi ulivyo akisema utamruhusu kila m,moja kufurahia haki na uhuru wake.

Rais aliyasema haya wakati mswada huo uliozaliwa kutokana na handisheki baina yake na Mpinzani wake Raila Odinga kukumbwa na hali ya sintofahamu baada ya Mahakama Kuu kuufutilia mbali.

Akiongea katika kaunti ya Kilifi wakati akitoa hati miliki kwa wenyeji Alhamisi, Julai 22, Uhuru alisema kando na kuruhusu kila mtu kufurahiya haki na uhuru, BBI pia itahakikisha kila mmoja anawakilishwa serikalini.

"Ndio maana nasisitiza kwamba tuupasishe mchakato wa BBI ndiposa kila Mkenya afurahie haki yake, uhuru na kila mmoja apate kusikilizwa," alisema.

Awali iliripotiwa kuwa katika uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watano mnamo Alhamisi, Mei 13, mchakato wa BBI ulitangazwa kuwa haramu na uliokiuka katiba.

Read also

Magazeti Ijumaa: Babu wa Miaka 93 Afunga Ndoa na Kipusa wa Miaka19

"BBI ilikuwa mradi wa rais ambao ni kinyume na Kifungu cha 257 cha katiba. Jopo lililoteuliwa na rais Uhuru Kenyatta halikuwa na mamlaka ya kusimamia shughuli ya marekebisho ya katiba," majaji walisema.

Mahakama ilisema kuwa hatua ya kuandaa safari ya kufanyia katiba marekebisho ni kinyume na katiba.

Majaji hao pia walikosoa pendekezo la BBI kubuni maeneo bunge mapya sabini wakishikilia kwamba jukumu hilo ni la tume ya uchaguzi na mipaka na sio la jopo lililoteuliwa na rais Kenyatta.

Baadaye wakereketwa wa BBI waliwasilisha kesi katika mahakama ya rufaa kufuatia uamuzi huo uliobatilisha mswada huo.

Mahakama hiyo itatoa uamuzi wake mnamo Ijumaa, Agosti 20.

Rais wa mahakama hiyo Daniel Masinga alisema kuwa jopo la majaji watakaoshughulikia kesi hiyo watahitaji muda ili kupitia stakabadhi zilizowasilishwa mahakamani na pande zote husika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.



Read also

Magazeti ya Alhamisi, Julai 15: Kijana Asimulia Namna Aliwaua Watoto 13 Nairobi
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke