Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru anyenyekea kwa Maulana, aamua kuliombea taifa

E4c92868447a9aaa Rais Uhuru anyenyekea kwa Maulana, aamua kuliombea taifa

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais alikuwa katika eneo la maombi Kitui ambapo alinyenyekea kwa MaulanaAliwataka Wakenya kuendelea kuombea taifa ili liweze kuafikia malengo yakeUhuru aliwataka wanasiasa wawe kama viongozi wa kanisa ambao hufanya kazi pamojaRais Uhuru Kenyatta Ijumaa Juni 25 aliamua kuombea Wakenya na taifa alipokuwa katika kanisa katoliki la Our Lady of Protection Shrine, Museve kaunti ya Kitui.

Rais alikuwa kaunti ya Kitui kuhudhuria kufunguliwa kwa eneo la maombi la Marian chini ya dayosisi ya Kitui.

Rais alionekana kwenye eneo hilo akituma maombi yake kwa Mwenyezi Mungu huku akiwataka Wakenya kufuata nyayo hizo.

"Rais Uhuru Kenyatta amewataka Wakenya kuendelea kuombea amani na umoja humu nchini aksiema hiyo ndiyo njia ya pekee ya kuafikia malengo ya taifa," taarifa ya Ikulu ilisema kuhusu ombi la Rais.

Rais alijiepusha na siasa wakati wa hafla hiyo na kuwataka wanasiasa humu nchini kupata funzo kutoka kwa viongozi wa kanisa ili wafanye kazi pamoja.

"Amewapa changamoto wanasiasa nchini kuwaiga viongozi wa kanisa na wafanye kazi pamoja kwa ajili ya maslahi ya Wakenya wote," aliongeza Rais.

Rais aliandamana na viongozi wa ukambani Kalonzo Musyoka, Charity Ngilu pamoja na Waziri Monica Juma na gavana wa benki kuu Patrick Njoroge.

Gavana Ngilu alihubiri haja ya viongozi wa mrengo wa NASA kuungana akisema anajua Rais Uhuru ana hofu kuhusu atakayechukua usukani baada yake.

"Mimi ni kiongozi wa miaka mingi na nikiangalia najua Rais hutaki kuacha nchi katika mikono ya mtu fulani. Hilo ninajua kwa sababu ataharibu nchi," Ngilu alisema.

Awali kumekuwa na ripoti za Rais kuwa na mpango wa kuunga muungano wa NASA mkono kwenye kivumbi cha kuingia Ikulu 2022.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke