Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru alivyowaacha Wakenya kwa furaha Mashujaa yake ya mwisho

9dd82fb48cb6198f Rais Uhuru alivyowaacha Wakenya kwa furaha Mashujaa yake ya mwisho

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Alhamisi Oktoba 21 yameangazia zawadi ambazo Rais Uhuru Kenyatta aliwapa Wakenya wakati wa kusherekea Mashujaa.

Ilikuwa ni Mashujaa Dei ya mwisho kwa Rais kwani mwaka ujao Ikulu itakuwa na mwenyeji tofauti.

1. Star

Gazeti la Star limeangazia mazuri ambayo Rais aliahidi Wakenya siku ya Mashujaa kama nji za kupiga jeki uchumi kutokana na athari za Covid-19.

Sekta ya elimu ndiyo itanufaika pakubwa huku serikali ikitoa KSh 8bn ili kujenga madarasa mapya kuwezesha masomo ya CBC.

Sekta za kahawa na majani chai zilipigwa jeki kwa kupokea KSh 1bn kila moja huku shilingi 1.5Bn zikirushwa katika sekta ya sukari.

Aidha gazeti hili limeangazia naibu rais William Ruto ambaye alimsifu Rais pakubwa wakati wa hotuba yake licha ya tofauti zao za kisiasa.

2. People Daily

Wakenya walipokea hatua ya Rais kuondoa kafyu ambayo imekuwepo tangu Machi 27, 2020 wakisema itasaidia pakubwa kujenga uchumi.

Aidha gazeti hili limeangazia hotuba za vigogo wakati wa Sherehe za Mashujaa ambapo naibu rais William Ruto alijipigia debe na kuahidi Rais kuwa ataendeleza kazi yake akichaguliwa rais.

Kinara wa ODM Raila Odinga naye alitumia nafasi yake kuelezea urafiki ambao amekuwa nao na eneo la Mt Kenya huku akiwakumbusha wakazi kuhusu 2002 aliposema Kibaki Tosha.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke