Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru alijua Ruto atazuiwa uwanja wa ndege

68e82c8e24cd83be Aliyekuwa mbunge wa Mukurweini Kabando wa Kabando

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ruto alikuwa na wakati mgumu pale Wilson baada ya maafisa kumwambia aombe ruhusu kabla ya kuondoka nchiniKabando anasema mtu wa kulaumiwa kutokana na hilo ni Rais Uhuru mwenyewe na wala si maafisa wengine serikaliniAkizungumza Jumatano alisema kilichotokea ni njama iliyopangwa ili kumdunisha na kuzua uhasamaTukio la Naibu Rais William Ruto kuzuiliwa kusafiri nchini Uganda linazidi kuzua hisia mseto za kisiasa.

Aliyekuwa mbunge wa Mukurweini Kabando wa Kabando alisema Rais Uhuru Kenyatta alikuwa na habari kuhusu aliyokuwa anapitia naibu wake.

Tukio hilo lilifanyika katika uwanja wa ndege wa Wilson Jumatatu na limezua cheche kali za kisiasa.

"Anajua kila kitu. Ni makosa kulaumu wengine kutokana na kilichofamfanyikia Ruto wakati wa safari yake," alisema Kabando katika mtandao wake wa Twitter.



Kabando alisema kilichotokea ni kwa sababu kuna matatizo kati ya Uhuru na Ruto na akaonya huenda mambo yakakuwa mabaya zaidi.

Kulingana naye, ni wazi sasa kuwa Rais ameamua kukabiliana na naibu wake kama njia ya kumuadhibu kisiasa.



Read also

Mpeni William Ruto Amani Baada ya Kumpokonya Majukumu Yake, Oscar Sudi

"Ukweli ni kuwa Rais ameamua kumuadhibu Naibu wake. Mambo yatakuwa mabaya zaidi hivi karibuni. Ruto ni lazima ajiandae kwa hali ngumu zaidi," alisema mwanasiasa huyo.

Kwa mujibu wa Kabando, naibu rais anafaa kumjulisha mdosi wake kila wakati anapopanga kuondoka humu nchini kwa ziara yoyote.

Akiongea na redio ya Inooro Jumatano asubuhi, Ruto alisema kilichotokea ni njama tu ya maafisa fulani wa serikali kujaribu kumdunisha.

"Nimekuwa naibu rais kwa miaka tisa na wakati wote huo nimekuwa nikisafiri katika nchi mbali mbali na hakuna wakati hata mmoja ambapo nimetakiwa kuomba ruhusa kutoka kwa mtu yeyote. NI Jumatatu tu hilo lilifanyika. Ni sheria gani hii ambayo imeanza kufanya kazi hivi karibuni?

"Hili lilifanywa ili kuleta uhasama lakini nimeliachiwa Mwenyezi Mungu," alisema Naibu Rais.

Alisema alikuwa akielekea Uganda kukutana na Rais Yoweri Museveni na haoni tatizo lolote kwani rais huyo ni rafiki wa Kenya.

READ ENGLISH VERSION



Read also

William Ruto: Sijawahi Hitaji Ruhusa Kutoka kwa Yeyote Kusafiri Nje ya Nchi

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke