Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru akerwa na wapiga picha jukwaani "Mashujaa Day"

71c387632ab7e073 Rais Uhuru akerwa na wapiga picha jukwaani "Mashujaa Day"

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru alikerwa na kundi la wapiga picha wa VIPs ambao walionekana kuzua mtafaruku kwenye jukwaa. Kenytta alionekana akiashiria kwa mkono kuwa wapiga picha hao wanafaa kuondolewa katika jukwaa.

Walinzi wa Rais walifanya hima kuondoa wapiga picha hao huku Uhuru akilazimika kusubiri sekunde chache kabla ya kuendelea na salamu zake.

Wapiga picha wa VIPs Jumatano Oktoba 20 walionekana kumkera Rais Uhuru Kenyatta kwenye jukwaa.

Rais aliwasili na kama kawaida baada ya kukagua guaride la heshima akaingia jukwaani kuwasalimia wageni.

Hata hivyo, kundi la wapiga picha liliandamana naye ili kunasa salamu zake kwa wageni waliokuwepo.

Wapiga picha hao hata hivyo walionekana kuleta msongamano katika jukwaa na hivyo kuzua hali ya sintofahamu.

Ilimlazimu kwa wakati mmoja kusimama kwanza ili kusibiri wapiga picha hao kusonga mbele na ilikuwa wazi amekerwa kama vile anaonekana akitumia mkono wake kuashiria waondolewe.





Ni tukio ambalo linamfanya Mama Rachael Ruto, ambaye yuko karibu na Rais, kuonekana kuingiwa na wasiwasi.

Hali ni kama hiyo kwa Spika wa Bunge Justin Muturi ambaye alikuwa akisubiri salamu zake Rais.

Katika taarifa nyingine, picha ya Rais na naibu wake imepepea mitandaoni baada ya wawili hao kuonekana wakitabasamu pamoja.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke