Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru ahidi kuondoa lockdown, masharti mapya ya COVID-19

Kenyan President Uhuru Kenyatta Rais Uhuru ahidi kuondoa lockdown, masharti mapya ya COVID-19

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba huenda akaondoa kafyu wakati wowote. Hii ni baada ya asilimia kubwa ya Wakenya kumrai kufanya hivyo ili kufungua uchumi wa nchiAidha, Uhuru amewasihi Wakenya wazidi kuzingatia masharti yaliyowekwa ya kuzuia msambao wa virusi vya COVID-19.

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kwamba huenda akaondoa kafyu wakati wowote bada ya kushinikiziwa na Wakenya

Uhuru alisema alisema amesiki kilio cha Wakenya na anajipanga jinsi atakavyoondoa kafyu ya kutoka saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri.

Rais aliyasema haya akiwa eneo la Sagana siku ya Jumatatu, Oktoba 18," Siku zijazo hata hamtakuwa na haja nayo, nafikiria kuondoa kafyu lakini sitasema ni lini, ila nitatangaza siku yoyote,"

Akionekana kutoa matamshi ya kejeli, Uuru alisema kwamba kafyu imewasaidia wanandoa wengi kuzalishawatoto, jamboambalo anafurahia sana.

" Nimefurahia kusema kwamba nimeridhika, kwa sababau siku hizi mnaenda nyumbai mapema kuzaani ama mwadhani kwamba mtapiga kura kesho msipozaana? Alisema Uhuru.

Awali, Rais Uhuru alikuwa amesema kwamba hataondoa kafyu kwa sababu ilikuwa inawasaidia Wakenya wengi hasa wanandoa kuafikiana na kutatua masuala ya kindoa.

" Kulingana na kile nimekiona hapa Kahawa Garison, nimeonelea kwamba kafyu iendelee,Watoto mumejaza hapa wengi," Uhuru alisema. Tunataka Kenya iendelee hivyo, Mungu atubariki na watoto wengi,"Uhuru alisema.

Aidha, Uhuru amewasihi Wakenya waendelee kuzingztia masharti yaliowekwa ya kuzuia msambao wa virusi vya Covid -19.

Uhuru alisema itakuwa rahisi kwa serikali kufungua unchumi iwapo tu Wakenya wataendele kuzingatia masharti yaliowekwa ya kudhibiti msambao wa virusi hivyo.

"Lazima ujikinge kutokana na ugonjwa huu ili tunpofungua nchi, kusiwe na vifo zaidi na mtakuwa huru kuishi ya kawaidi jinsi mnavyotaka," Uhuru aliongezea.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke