Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru afuta ziara yake ya siku tatu eneo la Ukambani

A9198c978c5724d9 Rais Uhuru afuta ziara yake ya siku tatu eneo la Ukambani

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ziara hiyo ambayo ilikuwa imeratibiwa kuanza Jumanne, Julai 6 hadi Alhamisi, Julai, 8, ilifutwaDuru zinarifu kwamba ziara hiyo ilifutwa kutokana malumbano miongoni mwa viongozi wa eneo hiloRais Uhuru alikuwa anatazamiwa kutembelea kaunti za Machakos, Makueni na Kituyi wakati wa ziara hiyo

Rais Uhuru Kenyatta mnamo Jumatatu, Julai 5, aliahirisha ziara yake ya siku tatu katika eneo la Ukambani kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Hata hivyo, duru zinarifu kwamba ziara hiyo ambayo ilikuwa imeratibiwa kuanza Jumanne, Julai 6 hadi Alhamisi, Julai, 8, ilifutwa kutokana malumbano miongoni mwa viongozi wa eneo hilo.

Pia imeibuka kwamba viongozi hao walikuwa wanavutana kuhusu maeneo ambayo rais angelizuru na miradi ambayo angelizindua.

"Ziara hii imeahirishwa kwa sababu hatujaonyesha umoja.Tofauti hizi zinachochewa na baadhi ya wanasiasa ambao hawakuwa katika Ikulu ya Nairobi tulipokutana na Rais," alisema mbunge mmoja wa eneo hilo ambaye jina lake lilibanwa kama ilivyoripoti Taifa Leo.

Kumekuwa na mvutano kati ya makundi mawili ya viongozi wa Ukambani kuhusu ziara hiyo ya rais moja linalomuegemea kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na lingine linalounga mkono Muungano wa Kiuchumi wa Kusini Mashariki mwa Kenya (SEKEB).

Viongozi wa Ukambani na hisia kinzani kuhusu ziara ya UhuruRais Uhuru alikuwa anatazamiwa kutembelea kaunti za Machakos, Makueni na Kituyi wakati wa ziara hiyo huku viongozi wakiwa na maoni tofauti.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua na mwenzake wa Makueni Kivutha Kibwana walitumia nafasi hiyo kumtupia Kalonzo vijembe wakisema:

“Tunatumahi ziara hiyo itatoa fursa ya miradi ya maendeleo na wala sio nafasi ya viongozi wazembe kuonekana wakitembea na kiongozi wa taifa," alisema Mutua.

Gavana Kibwana: "Wacha Rais atembee na mjumbe wa AU Raila Odinga kwa sababu amesimai amiradi kahaa ya barabra ene letu na pengine mtu mwingie yeyote anayetaka kuja,"

Gavana Charity Ngilu naye alisema wanatarijia bajeti iliyowaislsihwa Bungen mwezi jana itafaidi eneo hilo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke