Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru afungua rasmi Ikulu ya Machakos iliyojengwa na Gavana Mutua

34cfa9e6f84c879a Rais Uhuru afungua rasmi Ikulu ya Machakos iliyojengwa na Gavana Mutua

Tue, 13 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ofisi hiyo nzuri ya Ikulu ya Machakos iligharimu kaunti KSh 350 milioni na ilijengwa ndani ya miezi tisaGavana Mutua anasemekana kupata msukumo wa kujenga ofisi hiyo ya kisasa kutoka MarekaniSherehe kuu ya ufunguzi ilishuhudiwa na Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi wa ODM Raila Odinga na viongozi wengine Ijumaa, Julai 9Gavana wa Machakos Alfred Mutua hatimaye amefungua rasmi Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Machakos na ofisi ya gavana "White House".

Sherehe hiyo kuu ya ufunguzi ilishuhudiwa na Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi wa ODM Raila Odinga na kinara wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka Ijumaa, Julai 9.

"Ninapenda kuwashukuru viongozi wote waliopongeza kufunguliwa rasmi kwa Kituo cha Mikutano cha Machakos cha kisasa (na cha kutengeneza pesa) (kilichoko kwenye Hifadhi ya Watu maarufu) na ofisi ya Gavana wa Machakos (" Ikulu ") na Rais Uhuru Kenyatta. Ahsante sana Rais UK," aliandika.



Read also

Magazeti Jumanne, Julai 13: Maseneta Wataka Chanjo ya COVID-19 kuwa Lazima kwa Wakenya

Ikiitwa "Ikulu" kwa sababu ya kufanana kwake na Ikulu ya Marekani, ofisi hiyo nzuri inasemekana kuigharimu kaunti hiyo KSh 350 milioni na ilijengwa ndani ya miezi tisa.

Imejengwa kwenye kipande cha ardhi huko Masaku, ofisi hiyo ya kaunti ina mwonekano mzuri na unaweza kuiona kutoka mbali, na huenda ukadhani ni Ikulu ya jijini Nairobi.

Walakini, Mutua anasemekana kupata msukumo wa kujenga ofisi hiyo ya kisasa kutoka Marekani.

Ofisi hiyo ina pande mbili, Magharibi (West Wing) kutakapokuwa na ofisi ya gavana, mkuu wake wa wafanyikazi na ukumbi wa mikutano ya watendaji wakuu, na Mashariki (East Wing) kutakapokuwa Ofisi ya Mke wa gavana, washauri wa gavana na wafanyakazi wengine wa watakaokuwa wakifanya kazi humo.

Ukubwa wake ulifanya baadhi ya watu kuteta na kukosoa mitandaoni. Makao makuu hayo ya kaunti yakawa gumzo lilipozinduliwa mnamo Mei 6, 2020.



Read also

Tharaka Nithi: Watu Watatu Wafariki Dunia Baada ya Kunywa Pombe ya Asali

Mwanahabari Yvonne Okwara alidokeza kuwa serikali ya kaunti ya Machakos iliwafelisha wakazi wake kwa kujenga ofisi ya gavana.

Yvonne aliendelea kuuliza ikiwa jengo la kifahari lililojengwa kwa kipindi cha miezi tisa tu ndilo jambo la dharura zaidi kwa wakazi kipindi hiki.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke