Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru aamuru polisi kuharakisha uchunguzi wa mauaji ya Agnes Tirop

63658f22d3f21879 Rais Uhuru aamuru polisi kuharakisha uchunguzi wa mauaji ya Agnes Tirop

Wed, 13 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta ameamuru maafisa wa polisi kuharakisha uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanariadha Agnes Jebet Tirop.

Duru ziliarifu kwamba marehemu alikuwa na mizozo ya kinyumbani na mumewe mwenye utata.

Agnes Tirop alipatikana ameuawa nyumbani kwake huko Iten, kaunti ya Elgeyo MarakwetUhuru Kenyatta alimuomboleza Tirop kama shujaa na bingwa wa Kenya ambaye kifo chake ni pigo kubwa kwa idara ya michezo nchini.

Dada huyo ambaye ni bingwa wa mbio za mita 5,000 katika Olimpiki za Tokyo za 2020 alipatikana akiwa ameuawa nyumbani kwake huko Iten, kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Katika ujumbe wake wa rambirambi, kiongozi wa taifa alimuomboleza Tirop kama shujaa na bingwa wa Kenya ambaye kifo chake ni pigo kubwa kwa idara ya michezo nchini.

"Ninasihi idara za usalama zikiongozwa na Huduma ya Polisi ya Kitaifa kufuatilia na kuwakamata wahalifu waliohusika na mauaji ya Agnes ili wakabiliane na nguvu zote za sheria," Uhuru aliagiza.

Kulingana na mwenyekiti wa Riadha nchini Kenya katika Mkoa wa Nairobi Barnaba Korir, mwili wa Tirop ulipatkana na majeraha ya kisu tumboni.

Duru ziliarifu TUKO.co.ke kwamba marehemu alikuwa na matatizo ya ndoa na mumewe Emmanuel Ibrahim Kipleting ambaye walikuwa wametengana.

Kipleting ambaye alikuwa kocha wake anashukiwa kuwa mhusika mkuu katika mauaji hayo. Mnamo Septemba 12, 2021, marehemu alivunja rekodi ya wanawake ya kilomita 10 ambayo ilishikiliwa na Asmae Leghzaoui wa Morrocco.

Katika Olimpiki za Tokyo za 2020, Tirop aliibuka wa nne katika fainali za wanawake za mita 5,000 baada ya kutumia muda wa 14: 39.62.

Katika mbio hizo, Sifan Hassan wa Uholanzi aliibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 14: 36.79. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25, mnamo 2019, alishinda shaba katika mbio za mita 5000.

Mnamo mwaka wa 2015, alishinda tuzo za Mashindano ya Cross Country Championships.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke