Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru Kenyatta atoa msaada wa KSh 1 milioni kwa familia ya Mama Sarah Obama

0fgjhs4crs0u4uesc Rais Uhuru Kenyatta atoa msaada wa KSh 1 milioni kwa familia ya Mama Sarah Obama

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kufuatia kifo cha Mama Sarah Obama, ambaye alikuwa na umri wa miaka 99, Rais Uhuru Kenyatta ametoa mchango wake wa kibinafsi KSh 1 milioni kwa familia yake.

Uhuru ambaye hakuweza kuhudhuria hafla ya mazishi ya Mama Sarah, aliwakilishwa na Waziri wa Ulinzi Racheal Omamo.

Kwenye hotuba yake Uhuru alimtaja mwendazake kama Mama aliyewajali wajane na watu maskini katika jamii.

Aidha, rais Kenyatta amekitaja kifo cha mama Obama kama pigo kubwa kwa taifa na atakumbukwa kwa kuwakaribisha watalii humu nchini kutoka mataifa mbali mbali.

"Ukarimu wake ulimuwezesha kupokea wageni kutoka sehemu mbali mbali duniani. Kwa hivyo taifa linaomboleza mtu ambaye alijitolea kuongoza na kuhakikisha ndoto ya wengi inatimia, kwa hivyo wacha tusherehekee yale aliyoweza kutimiza wakati alipokuwa hai. Ni maombi yangu kwamba mungu atatutia nguvu wakati huu ambao taifa limepoteza" Ujumbe wa Rais Kenyatta

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke