Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru Kenyatta aondoka nchini kwa ziara ya siku 3 DRC

15ae25b82fd9324c Rais Uhuru Kenyatta aondoka nchini kwa ziara ya siku 3 DRC

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta ameondoka nchini na anasemekana yuko katika ziara rasmi ya kibiashara katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa siku kadhaa

TUKO.co.ke imefahamishwa kwamba Uhuru alialikwa na Rais wa nchi hiyo na maraisa hao wawili wanatarajiwa kujadili maswala ya hapa na pale yanahusiana na biashara na maendeleo.

Uhuru aliandamana na viongozi kadhaa akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Raychelle Omamo, mwenzake wa Ugatuzi Eugene Wamalwa, Balozi wa Kenya mjini Kinshasha George Masafu na viongozi wengineo.

Ziara za Uhuru nchini Kongo inajiri siku moja baada ya Rais wa Somalia Mohammed Fatmajo pia kufanya mkutano wa kibiashara na rais wa nchi hiyo.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke