Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru Kenyatta amesema "Njaa" imekua janga la taifa

0fgjhs3e6aq7a4v4fg Rais Uhuru Kenyatta amesema "Njaa" imekua janga la taifa

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumatano, Septemba 8, ametangaza baa la njaa kuwa janga la kitaifa katika sehemu kadha za nchi.

Uhuru ametaka wizara ya fedha na ya Usalama wa Ndani kusadia familia ambazo zimeathirika na janga hili kwa kuzipa chakula na maji.

Msemaji wa Ikulu Kanze Dena amesema uamuzi huu umetolewa baada ya Rai kukutana na viongozi 85 kutoka sehemu ambazo zimeathirika sana.

" Maelekezo zaidi kuhusiana na jinsi janga hili litakavyo shughulikiwa na serikali yatawekwa wazi hivi karibuni." Kanze alisema.

Kaunti ambazo zimeathirika na baa la njaa ni Marsabit, Garissa, Kilifi, Taita Taveta, Embu, Meru, Nyeri, Samburu, Tana River, Kitui na Kajiado na imeripotiwa kwamba hali hii itaendelea kwa zaidi ya miezi minne.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke