Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Uhuru: Huenda uchaguzi wa 2022 ukaahirishwa baada ya uamuzi wa BBI

3b11375c1b5268ca Rais Uhuru: Huenda uchaguzi wa 2022 ukaahirishwa baada ya uamuzi wa BBI

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta amesema huenda uamuzi wa mahakama kuhusu mswada wa BBI ukaathiri uchaguzi mkuu ujao. Mahakama ilisema IEBC haina makamishana wa kutosha kutekeleza wajibu wake kikatiba na hivyo kutuoa BBI.

Rais anasema hilo lina athari kwa uchaguzi mkuu ujao kwani tafsiri ni kuwa IEBC haiwezi kutekeleza wajibu huoAlisema ni suala ambalo sasa linabidi kusubiriwa kuona vile mambo yataendelea baada ya uamuzi huo

Akiongea kwenye mahojiano na wahariri katika Ikulu Agosti 23, Rais alisema uamuzi wa majaji wa Mahakama ya Rufaa kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC haina makamishna wa kutosha utaathiri uchaguzi ujao.

"Sina chochote cha kusema kuhusu kuwepo njama ya kuahirishwa uchaguzi ujao, lakini kama tutafuata kile Mahakama ya Rufaa iliamua kuhusu IEBC, yale wanatuambia ni kuwa hatutakuwa na uchaguzi 2022 kwa sababu IEBC haina idadi ya kutosha ya makamishna," alisema Kenyatta.

Rais alisema kwa sasa ameamua kwanza kuangali mambo akiwa kimya ili kuona ni lipi litatokea kutokana na uamuzi huo wa mahakama.



"Sitaki kusema mengi kuhusiana na suala hilo, wacha tuone vile mambo yataendelea," alisema Rais.

Aliongeza kuwa yeye yuko tayari kumaliza kipindi chake kwa mujibu wa katiba na kuondoka tofauti na madai ambayo yamekuwepo kuhusu njama ya kuendelea kukaa mamlakani.

"Kama vile mimi nimekuwa nikisema, niko tayari uchaguzi ufanyike kwa mujibu wa mpangilio na hilo ni Agosti 9," aliongeza Kenyatta.

Wakati wa kutoa uamuzi wao kuhusu rufaa ya BBI, majaji sita wa mahakama ya Rufaa walikubaliana na wenzao wa Mahakama ya Juu kuwa IEBC ilikosa makamishana wa kutosha ili kuendesha shughuli ya kuchambua sahihi za BBI.

Majaji hao walisema haina 'quorum' na hivyo ilichokuwa ikifanya ni kinyume cha katiba na ndipo suala hilo likawa kigezo kimoja cha BBI kutupwa nje.

Ni uamuzi ambao umeibua maswali kuhusu shughuli zote ambazo IEBC imekuwa ikitekeleza ikiwamo chaguzi ndogo kadhaa zilizofanyika.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, inamaanisha chaguzi hizo ndogo sasa zinaweza kutupiliwa mbali iwapo mlalamikaji atafika mahakama.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke