Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Tinubu aamuru wanafunzi waliotekwa waachiwe bila fidia

Rais Tinubu Aachilia Huru Maelfu Ya Wafungwa Nigeria Rais wa Nigeria, Bola Tinubu.

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ameamuru maafisa wa usalama kutolipa fidia kwa ajili ya kuachiliwa kwa zaidi ya wanafunzi 250 wa shule ya msingi waliotekwa nyara na watu wenye silaha wiki iliyopita.

VOA imeripoti kuwa, Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa habari nchini humo, Mohammed Idris, ambapo amesema, ndugu wa wanafunzi hao wanasema watekaji nyara wameomba fidia kubwa ili kuwaachilia wanafunzi waliotekwa nyara shuleni mwao Alhamisi iliyopita katika kijiji cha Kuriga kaskazini magharibi mwa Jimbo la Kaduna.

Katika miaka mitatu iliyopita, mamia ya wanafunzi walitekwa nyara. Waathirika wa utekaji nyara nchini Nigeria mara nyingi huachiwa huru baada ya mazungumzo na mamlaka, ingawa maafisa wanakanusha malipo ya fidia kufanyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live