Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Suluhu aomboleza kifo cha mbunge wa upinzani Khatib Said Haji

Ee26a08607bf2680 Rais Suluhu aomboleza kifo cha mbunge wa upinzani Khatib Said Haji

Thu, 20 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mbunge Khatib Said alifariki dunia Alhamisi Mei 20, 2021 akipokea matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Muhimbili

- Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai alituma rambi rambi zake kwa familia akisema amehuzunishwa na kifo cha mwanasiasa huyo

- Khatib Said Haji ni mbunge wa tatu kufariki dunia tangu bunge la 12 lilipoanza Novemba 2020, Martha Umbula akiwa mmoja wao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suhulu ameomboleza kifo cha mbunge wa upinzani wa eneo bunge la Konde Khatib Said Haji.

Haji alifariki dunia Alhamisi, Mei 20, 2021 akipokea matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Muhimbili nchini Tanzania.

" Ningependa kutangaza kifo cha mbunge wetu Khatib Said Haji kwa masikitiko, natuma rambi rambi zangu kwa jamaa, marafiki na wananchi wa Tanzania kwa jumla," Alisema Suluhu.

Rais Suluhu aliyasema haya akiwa kwenye kutano na rais wa Uganda Yoweri Museveni katika Ikulu ya Dar es Salaam.

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, Rais Museveni yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Agenda kuu ya mkutano huo ni kwa marais hao kushuhudia utiaji saini wa mikataba ya utelekeza wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Spika wa bunge la kitaifa la Tanzania Job Ndugai pia alituma salamu zake za pole kwa familia ya mwenda zake.

" Nime[okea taarifa za kifo cha mbunge Haji kwa mstuko na huzuni, ningependa kutuma rambi rambi zangi kwa waliofiwa ikiwemo familia, jamaa, marafiki na viongozi wa tabaka mbali mbali. Mungu atawafariji wote wakati huu wa majonzi na huzuni," Ndugai alisema.

Naibu spika wa bunge la kitaifa Tulia Ackson aliahirisha kikao cha bunge akisema ni kwa ajili ya kupeana nafasi ya mazishi ya mwenzao

Haji atazikwa mjini Pemba kabla ya saa kumi hii leo alasiri kulingana na desturi ya jamii ya kiislamu, viongozi wa tabaka mbali mbali wanatarajiwa kuhudhuria mazishi yake.

Marehemu alizaliwa mnamo tarehe 31 Julai mwaka wa 1962 mjini Zanzibar na amekuwa mbunge wa Konde tangu mwaka wa 2010.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke