Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Somalia atoa tamko kuhusu Al-Shabaab

Rais Somalia Aloshaaba Rais Somalia atoa tamko kuhusu Al-Shabaab

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesisitiza kuuwa, operesheni dhidi ya kundi la kigaidi la al-Shabab itaendelea hadi pale ushindi utakapopatikana.

Mohamud ameyasema hayo baada ya vikosi vya serikali kuondoka kwenye miji kadhaa kufuatia mashambulizi mabaya yaliyofanywa na al Shabab dhidi ya wanajeshi kwenye kijiji cha Cowsweyne hivii kkaribuni.

Kiongozi huyo amesifu wanajeshi wa serikali waliwafurusha wanamgambo kutoka ngome zao tangu kuanza kwa operesheni mwaka jana, huku akiwashukuru wanajeshi pamoja na wapiganaji walioshirikiana nao.

Duru za kiusalama zinaarifu kuwa, magaidi zaidi ya 3,000 wameuawa katika awamu ya kwanza ya operesheni za kulitokomeza kundi hilo hasa katika majimbo la Hirshabelle na Galmadug.

Wakati huo huo, kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kimesema kitawaondoa wanajeshi wengine 3,000 katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Kamanda wa ATMIS, Luteni Jenerali Sam Okiding alisema hayo jana Jumane mjini Mogadishu katika kikao na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, "Maandalizi ya awamu ya pili ya kuwaondoa askari 3,000 wa ATMIS nchini Somalia kufikia mwishoni mwa Septemba yanaendelea."

Somalia imekuwa ikipambana na ukosefu wa usalama tangu mwaka 1991 na imekuwa uwanja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi. Genge la kigaidi lililofanya ukatili mkubwa ndani na nje ya Somalia ni la al Shabab ambalo limejitangaza kuwa ni tawi la mtandao wa kigaidi wa al Qaida barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live