Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Somalia afunguka maamuzi ya UN kuhusu silaha

Somzlia Marufuku Silaha.jpeg Rais Somalia afunguka maamuzi ya UN kuhusu silaha

Sun, 3 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amepongeza uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kuiondolea vikwazo vya silaha nchi yake.

Rais huyo wa Somalia ambaye ameapa kupambana na kundi la wanamgambo wa al-Shabab amesisitiza kuwa, kuondolewa nchi hiyo vikwazo vya silaha ni hatua muhimu mno katika juhudi za kupambana na kundi la kigaidi la al-Shabab kwa ajili ya kurejesha amani na usalama nchini humo.

Pongezi hizo za Rais wa Somalia zinafuatia hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kuupasisha kwa kauli moja azimio la kuondoa vikwazo vya mwisho vya silaha dhidi ya serikali ya Somalia na vikosi vyake vya usalama.

Baraza hilo lenye wanachama 15 limepasisha maazimio mawili yaliyoandaliwa na kuwasilishwa na Uingereza: moja likiwa ni la kuondoa vikwazo kamili vya silaha kwa Somalia na lingine la kuweka tena vikwazo vya silaha kwa kundi la kigaidi la al Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa al Qaeda.

Wanamgambo wa al-Shabab wa Somalia

Azimio la kuondoa vikwazo vya silaha linaeleza kuwa linatekelezwa "kwa ajili ya kuepuka shaka, kwamba hakuna vikwazo vya silaha itakavyowekewa Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Somalia."

Kundi la kigaidi la al-Shabaab ambalo lina mielekeo ya itikadi kali na mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda, limekuwa likijaribu kuipindua serikali kuu ya Somalia tangu mwaka 2007 na limeshafanya operesheni nyingi za kigaidi na kuua idadi kubwa ya wanajeshi na raia wa nchi hiyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live