Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Sierra Leone kugombea muhula wa pili licha ya upinzani mkali

Rais Sierra Leon Rais Sierra Leone kugombea muhula wa pili licha ya upinzani mkali

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone anatazamiwa kugombea muhula wa pili wa urais katika uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika Juni 24.

Bio amejitosa kwenye kinyang'anyiro hicho licha ya makundi ya upinzani kufanya maandamano ya mara kwa mara, ya kumtaka aachie madaraka, wakimtuhumu kuwa ameshindwa kuliendesha taifa.

Nchi hiyo hivi sasa inakabiliwa na mfumko wa bei na gharama ya juu ya maisha, changamoto ambazo zimewafanya wapizani wakosoe utendaji kazi wa rais huyo mwenye umri wa miaka 59.

Agosti mwaka jana, rais huyo alisema maandamano ya ghasia yaliyopelekea kuuawa raia 21 na maafisa usalama wasiopungua sita mwezi huo yalikuwa ni sehemu ya jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali.

Mfumko wa bei za bidhaa nchini humo ulipanda kwa karibu asilimia 30 kipindi hicho, na kuwaongezea matatizo ya kiuchumi na kijamii akthari ya wananchi wa nchi hiyo yenye jamii ya watu milioni 8.

Uchaguzi mkuu kufanyika Jumamosi

Samura Kamara ambaye alikuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha upinzani cha All People's Congress (APC) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2018 nchini Sierra Leone, anatazamiwa kuteuliwa na vyama vya upinzani kugombea urais katika uchaguzi huo wa Jumamosi.

Wananchi milioni 3.4 wa Sierra Leon waliotimiza masharti ya kupiga kura wanatazamiwa kuelekea kwenye masanduku ya kupigia kura Jumamosi ya keshokutwa ya Juni 24 kumchagua rais, wabunge na viongozi wa serikali za mitaa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live