Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Watanzania jifunzeni kutoka Rwanda.

Rais Samia Rwanda Rais Samia:Tuko Tayari kujifunza Rwanda.

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo ni siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake rasmi nchini Rwanda. Alipokelewa jana na mwenzake Paul Kagame katika ikulu ya rais. Hii ni ziara ya kwanza ya rais Samia Suluhu Hassan nchini Rwanda baada ya mtangulizi wake John Magufuli kuzuru nchi hiyo kabla ya kifo chake, mwezi Machi. Nchi hizo mbili zina uhusiano mzuri.

Ziara ya rais wa Tanzania nchini Rwanda inalenga"kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili," amesema Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Wakizungumza na waandishi wa habari, baada ya kikao chao cha faragha, Rais Paul Kagame ameiahidi Tanzania kuwa Rwanda iko tayari kutoa ushirikiano kwa lolote ambalo linalenga maslahi ya pande mbili, ikiwemo kutafutia ufumbuzi matatizo yaliyotokana na janga la COVID-19.

Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza Rwanda kwa hatua iliyopiga katika sekta ya uchumi na mapambano dhidi ya COVID-19 na kuiapongeza Rwanda kwamba 'mko mbele yetu nasi tuko tayari kuja kujifunza kwenu, lakini yapo mambo ambayo yameingia sasa ya Covid-19, nayo tumeyazungumza kwa mapana yake, na tumeweka mikakati ya kushirikiana kupitia kituo chetu cha Rusumo lakini pia kama tulivyosaini mambo ya madawa. Tumekubaliana kuendeleza ushirikiano uliopo ambao ni ushirikiano wa kihistoria na wa kindugu. Asanteni sana'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live