Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia Ampa Kenyatta Korongo 20

Korongooo Korongo

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan, amempa Rais Kenyatta ndege 20 aina ya Korongo kutokana na Kenya kuwa na idadi ndogo ya ndege hao (Kenya inao 12 tu), hivyo mtalii ilimlazimu kuja Tanzania kuwaona kiuhalisia. Tanzania ina Korongo 4,000.

Mhe. Samia ametoa zawadi hiyo leo Ijumaa, Desemba 10, 2021 wakati akihutubia mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mashirikiano kati ya Tanzania na Kenya yaliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

“Katika Sekta ya Utalii ndugu zetu wakenya walikuwa wanaona ndege Korongo wakiwa Tanzania na pengine katika kutembeza watalii, mtalii alikuwa anaulizia hawa ndege lakini wao hawakuwa nao hivyo watalii walilazimika kuja Tanzania kumuona huyo ndege.

"Kenya wana ndege wachache sana aina ya Korongo ambao wapo Tanzania hivyo waliomba ndege hao kutoka Tanzania na leo nina furaha kumkabidhi Rais Kenyatta cheti maalum cha ndege 20 ambao tunawapeleka Kenya ili wakae kwenye mbuga zao. Taratibu zikitimia watafika kabla ya Christmas, hiyo ndio zawadi yetu….” –Rais Samia Suluhu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live