Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Ruto awachana wapinzani wake

RUTO RAILA SPLIT Ruto na Odinga

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya William Ruto amewataka wapinzani wake kisiasa kusahau na kuachana na mazungumzo yanayohusu uchaguzi na badala yake wajikite kutetea maslahi ya wananchi.

Rais Ruto amesema si haki baada ya uchaguzi wanasiasa kuwarudisha nyuma wananchi kwenye masuala yanayohusu uchaguzi na viongozi.

Ruto amesisitiza kuwa wananchi walifanya chaguo lao katika mchakato wa kidemokrasia na walikuwa na hamu ya kuona viongozi wakitekeleza majukumu yao.

“Hatuwezi kuendelea kuzungumzia uchaguzi, ni wakati wa kuzungumza na kupanga mipango ya maendeleo ambayo yatabadilisha maisha ya wananchi,” alisema Rais Ruto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live