Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Ruto avunja baraza lake la mawaziri

Rais Rutoooo Rais Ruto avunja baraza lake la mawaziri

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais William Ruto amelivunja baraza lake la mawaziri isipokuwa kwa nafasi ya Kiongozi wa mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje, Musalia Mudavadi.

Uamuzi huo wa Rais Ruto ameutangaza leo, Alhamisi Julai 11, 2024 nchini Kenya akisema mabadiliko hayo yatasaidia kuunda serikali itakayosaidia kuongoza kasi ya utekelezaji wa mipango ya kukabiliana na changamoto nyingi zinazowakabili wananchi.

Katika hotuba yake hiyo iliyopokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kenya hususan vijana maarufu (GEN Z), Ruto amesema, licha ya kuvunja baraza hilo nafasi ya Naibu wa rais haijaathiriwa na mabadiliko hayo pia.

Uamuzi huo alioutangaza Rais Ruto unahusishwa moja kwa moja na maandamano ya vijana wa Kenya waliokuwa wakipinga Muswada wa Sheria wa Bajeti Kuu ya Nchi hiyo ambao ulilalamikiwa kwakuwepo na ongezeko kubwa la kodi litakalomuumiza mwananchi wa kawaida na hivyo Rais Ruto kukataa kuusaini na kuurejesha muswada huo bungeni.

Hata hivyo Rais Ruto amesema itamchukua muda kufanya majadiliano ya kuunda baraza jipya la mawaziri litakalohusika na uendeshaji wa serikali suala lililopokelewa na maoni mseto kutoka kwa wananchi.

Rais Ruto amesema baraza hilo litaangalia namna ya kusaidia kuongeza ufanisi na kasi ya kukabiliana na mzigo wa madeni, kuongeza rasilimali za ndani, kupanua nafasi za kazi, kuondoa ubadhirifu wa fedha, kupunguza gharama na matumizi makubwa ya serikali na kukomesha ufisadi wa fedha za umma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live