Rais William Ruto amesema Serikali itafanya mabadiliko kwenye gharama za matibabu kwa Wananchi wa kipato cha chini wanaotumia Bima ya Mfuko wa Bima wa Taifa (NHIF) ambapo waliokuwa wanalipa Tsh 8,201 kwa mwezi wataanza kulipa Tsh. 4,921.
Ruto ameongeza kuwa Wananchi ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za Matibabu, Serikali inakamilisha mpango wa kutambua hali ya kipato cha kila Mwananchi na itabeba gharama zote ili watibiwe bure.
Amesema; "Kila Mwananchi kwa umoja wetu tutaenda Hospitali na tutatibiwa bila ya kuulizwa Pesa yoyote kwasababu tunataka kuhakikisha kwamba Kenya ni Nchi ya Usawa."
Utekelezaji wa mpango huo unatokana na Kenya kupitisha Sheria ya kila mfanyakazi kukatwa 2.75% ya Mshahara kila mwezi ili kuchangia gharama za uendeshaji wa NHIF.