Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Ruto amtuhumu Kenyatta kufadhili maandamano Kenya

Kenyatta Pic Jino Kwa Jinooo Rais Ruto amtuhumu Kenyatta kufadhili maandamano Kenya

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto amemtuhumu mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta kuwa anafadhili maandamano ya upinzani nchini humo na kumuonya kuwa ikiwa ataendelea kufadhili shughuli za Azimio, atalazimika kumchukulia hatua.

Dkt Ruto ameyasema hayo leo Julai 14, 2023, katika kaunti ya Nakuru na kubainisha kuwa Kenyatta alikuwa akiwafadhili vijana wa Mungiki kufanya fujo wakati wa maandamano ya Azimio la Umoja nchini humo huku akimtaka kuwa muungwana na kuongeza kuwa yeye alimuunga mkono kipindi akiongoza nchi hiyo.

“Nikuombe rafiki yangu Uhuru, achana na huyo mzee (Raila), acha kutoa pesa za kuajiri mungiki kuiharibu Nairobi, wewe ulikuwa Rais tukakuunga mkono, tafadhali kuwa muungwana,” amesema Rais Ruto.

“Mimi nataka nimwambie rafiki yangu Uhuru hata wewe achana na huyu mzee. Wacha kumpea pesa ya kununua watu ya Mungiki wachome Nairobi. Usipowachana na yeye wewe tutakusafirisha na huyo kitendawili wako” ameongeza Dkt Ruto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live