Rais wa Iran Ebrahim Raisi amewasili nchini Kenya mapema Jumatano asubuhi kwa mazungumzo ya pande mbili na Rais William Ruto.
Raisi, ambaye ziara yake ya Kiserikali iliratibiwa Jumanne kabla ya kuratibiwa upya ghafla, alikaribishwa na Ruto katika Ikulu ya Nairobi.
Kiongozi wa Irani alikagua gwaride la heshima
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje, ratiba ya kiongozi huyo wa Iran ilipitiwa upya ili kuruhusu kukamilishwa kwa Makubaliano muhimu ya msingi ya kuendeleza uhusiano.
Ziara hiyo nadra ya Raisi barani Afrika ni sehemu ya juhudi za hivi punde za kidiplomasia za Iran kupunguza kutengwa kwa taifa hillo la Kiislamu kwa lengo la kuunda ushirikiano mpya.