Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Ramaphosa mbele ya kamati ya uchunguzi kuhusu ufisadi

Cyril Ramaphosa?fit=754%2C409&ssl=1 Rais Ramaphosa

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa leo Jumatano, Agosti 11, 2021, anatarajiwa kufika mbele ya jopo la uchunguzi wa madai ya ufisadi dhidi ya mtangulizi wake Jacob Zuma.

Jopo hilo lilianzishwa kuchunguza madai kwamba mtangulizi wake Jacob Zuma wakati wa kipindi chake uongozini – aliruhusu familia tajiri ya Gupta kupora rasilimali za serikali na kushawishi seraza serikali na uteuzi wa baraza la mawaziri.

Wote wawili Zuma na Gupta wanakanusha makosa yoyote. Ufisadi huo unakadiriwa kugharimu Afrika Kusini $ 81bn (£ 58bn) fedha za umma na kupoteza fursa nyingi ambazo zingekuwa na manufaa kwa nchi.

Bwana Ramaphosa alikuwa naibu kiongozi wa chama kinachotawala ANC wakati huo. Ameitwa kujibu maswali juu ya kile chama kilijua, ikiwa kuna chochote, juu ya madai ya utovu wa nidhamu na ikiwa walifanya chochote kujaribu kuzuia uharibifu huo.

Chanzo: globalpublishers.co.tz