Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Ramaphosa aunga mkono kuachiwa kwa Zuma

Zuma2 Jacob Zuma, Rais wa zamani wa Afrika Kusini

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameunga mkono uamuzi wa kumwachilia Rais wa zamani Jacob Zuma wa kutumikia kifungo chake nyumbani kufuatia kuzorota kwa afya ya mstaafu huyo.

Aidha, Rais Ramaphosa amemtakia Zuma afueni ya haraka, wakati wa hotuba yake katika mkutano wa kamati kuu ya kitaifa ya chama tawala cha ANC.

“Tumesikia kuwa hayuko sawa na tungependa kumtakia afueni ya haraka kwani amerejeshwa nyumbani kwake kuwa na wapendwa wake, ”alisema.

Itakumbukwa kuwa, Septemba 05 mwaka 2021, Idara ya Huduma za Magereza ilitangaza kuwa Rais huyo wa zamani atatumikia kifungo cha miezi 15 iliyobaki nyumbani.

Hali ya ugonjwa wake haikuelezwa , lakini taarifa ilisema atakamilisha adhabu yake yote chini ya masharti maalum.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live