Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Ramaphosa ashtushwa Nabii Bushiri kutoroka

BUSHIRI AND CYRIL RAMAPHOSA Rais Ramaphosa ashtushwa Nabii Bushiri kutoroka

Fri, 20 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Rais wa South Africa Cyril Ramaphosa ameshtushwa na kitendo cha Nabii wa Malawi na Mke wake Mary kutoroka South Africa wiki iliyopita bila kutumia hati za kusafiria (passport), anafatilia ili waliohusika kuwatorosha waadhibiwe kisheria.

Baadhi ya Mitandao iliripoti kwamba kuna uwezekano walitoroshwa na Wezi wanaofanya biashara ya kusafirisha magari ya wizi huku mitandao mingine ikisema alitoroshwa kwa kutumia Ndege ya Rais.

Nabii Shepherd Bushiri na Mary ambae ni Mke wake wana kesi Mahakamani South Africa wakituhumiwa kulaghai na kutakatisha fedha Nchini humo.

Kwa sasa Nabii Bushiri pamoja na Mkewe wapo nchini Malawi na jana walijisalimisha katika vyombo vya dola nchini humo.

LIVE: MWINYI “ACT WAZALENDO TUMEWAANDIKIA BARUA”, BARAZA JIPYA HAKUNA MANAIBU WAZIRI

Chanzo: millardayo.com