Rais wa Rwanda Paul Kagame, akiwa ziarani jijini Conakry nchini Guinea, amekutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, Mamady Doumbouya.
Kiongozi huyo wa Rwanda, amesema nchi ya Guinea licha ya kuwa na changamoto hasa za kisiasa baada ya jeshi kuchukua madaraka, mwaka 2021 baada ya kumuondoa madarakani, rais Alpha Conde, hakuna kinachoshindikana, kuirejesha nchi hiyo kwenye mstari.
Aidha, ameelezea umuhimu wa nchi yake kufanya kazi kwa pamoja na Guinea ili kutatua changamoto zinazoyakumba matataifa hayo mawili.
Hii ni ziara yake ya pili nchini humo, baada ya kutembelea nchi hiyo mwaka 2016 na kutiliana saini mikataba ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, ikiwemo mashauriano ya kisiasa, afya, kuondoa VIZA na kushirikiana kwenye usafiri wa angaa.
Mbali na Guinea Conakry, Kagame pia ametembelea Benin na Guinea Buissau, ambapo jana Jumatatu alifanya mazungumzo na rais Umaro Sissoco Embaló. Akiwa nchini Benin, alitia saini mikataba tisa ya ushirikiano ukiwemo wa kijeshi.