Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Nigeria ataka mazungumzo na waandamanaji

4857035b9297073dba009e41c466b2a2 Rais Nigeria ataka mazungumzo na waandamanaji

Fri, 23 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Abuja,Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amewataka vijana wanaohusika na maandamano kusitisha mara moja ili waweze kusogea katika meza ya mazungumzo na Serikali.

Katika hotuba yake kwa Taifa hapo jana , ikiwa ni hotuba yake ya kwanza toka maandamano hayo yaanze, amewataka waandamanaji hao wasitumike na watu wenye nia mbaya wenye lengo la kuvuruga demokrasia ya nchi.

Hata hivyo, Buhari akugusia suala la waandamanaji kupigwa risasi na vikosi vya usalama ambapo watu wasiopungua 12 walipoteza maisha.

Maandamano hayo yalianza wiki mbili zilizopita mara baada ya kikosi cha jeshi la polisi nchini humo (SARS) kinachohusika kupambana na wizi wa kutumia silaha, ambacho kimekuwa kinashutumiwa kuwaweka watu kizuizini kinyume cha sheria na kushambulia raia kwa risasi jambo lililomshawishi Rais huyo kukivunja kikosi hicho mnamo Oktoba 11.

Chanzo: habarileo.co.tz