Katika tukio lisilo la kawaida, marais wa zamani wa Burundi Sylvestre Ntibantunganya na Domitien Ndayizeye wamefanya mazungumzo na Rais Evariste Ndayishimiye kuhusu maendeleo na uongozi wan chi, vimeripoti vyombo vya habari vya Burundi.
Ni nadra kwa kiongozi aliyeko madarakani nchini Burundi, na katika baadhi ya mataifa ya maziwa makuu kufanya mazungumzo na watanguli wake.
Mazungumzo ya Rais Evariste Ndayishimiye na marais wa zamani yalirekodiwapamoja na picha zaona kutangazwa Jumatatu.
Walizungumza kuhusu "utawala bora na maendeleo ya wananchi"
Kulingana naorodha ya kiwango cha maendeleo cha Umoja wa Mataifa (HDI), Burundi ni miongoni mwa nchi tano masikini zaidi duniani, lakini serikali ya Gitega haikubaliani na hilo.
Rais Evariste Ndayishimiye alisikika akiwaambia wananchi kuwa “Burundi ni moja ya nchi zinazoitunza dunia sana” na kwamba “hawahitaji dola”
Vyama vya upinzani nchini Burundi vinalaumu utawala wa chama tawala cha CNDD-FDD kwa kutokubali hali halisi ya wananchi na kuitafutia suluhu, na badala yake dkuonyesha picha nzuri ambayo sio halisi.