Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Nana ashinda muhula wa pili Ghana

99a14d505333b354e70bd93e26549eef Rais Nana ashinda muhula wa pili Ghana

Thu, 10 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo ameshinda muhula wa pili wa kiti hicho mara baada ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini humo usiku wa kuhamkia leo, huku mpinzani wake John Mahama akipinga matokeo hayo na kusema atakwenda mahakamani.

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Katika uchaguzi huo Akufo-Addo amepata asilimia 51.59 ya kura, akimpita kiongozi wa upinzani na Rais wa zamani wa taifa hilo Mahama aliyepata asilimia 47.36.

Licha ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuwa inasifika kwa demokrasia thabiti, Mahama anapinga matokeo hayo kutokana na chama chake kushinda viti vingi vya ubunge na kusema kuwa zoezi zima la mchakato wa uchaguzi liligubikwa na udanganyifu mkubwa.

Chanzo: habarileo.co.tz