Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Museveni kuwasaka walioua watalii wawili Uganda

Museveni Mdsh Rais Museveni kuwasaka walioua watalii wawili Uganda

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema Serikali yake itawasaka watu waliofanya uhalifu wa kuwaua wanandoa pamoja na mtembeza watalii.

Serikali ya Uganda imesema inawasaka watu hao waliofanya tukio hilo katika Mbuga ya Kitaifa ya Malkia Elizabeth nchini Uganda.

Rais Museveni, alilaani shambulizi hilo na kusema kuwa " Kitendo cha woga," na kuapa kwamba washambuliaji watalipa na maisha yao.

"Ilikuwa ni kitendo cha woga kwa upande wa gaidi kushambulia raia wasio na hatia na ya kusikitisha kwa wanandoa ambao walikuwa wapya na kuzuru Uganda kwenye fungate yao," Museveni aliandika kwenye X.

"Bila shaka, magaidi watalipa kwa maisha yao duni," aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live