Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba hayuko 4katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU kama inavyodaiwa .
Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa uvumi kuhusu hali yake ya kiafya kupitia mtandao wake wa twitter, rais Museveni alisema kwamba serikali yake ingetangaza iwapo angekuwa amelazwa katika chumba hicho.
Bwana Museveni alisema kwamba hajalala kwasababu ya kuwa mgonjwa katika nyumba yake isipokuwa kwasababu ya kupumzika tu.
‘’Pia niliona baadhi ya watu wachache kutoka, nadhani, Kenya, wakisema kwamba nilikuwa ICU n.k.Kama ningekuwa ICU, serikali ingearifu nchi. Kuna nini cha kuficha? Hata hivyo, sijalala kama mgonjwa nyumbani humu isipokuwa kulala, achilia mbali kulazwa hospitali, iwe ICU au vinginevyo’’.
Hatahivyo alimalizia ujumbe wake huo kwa kusema kwamba 'Endelea kuomba tutashinda'
Kumekuwa na uvumi katika siku chache zilizopita kwamba afya ya rais huyo haikuwa njema tangu atangazwe kwamba alikuwa akiugua virusi vya corona.