Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Mstaafu atupwa jela miaka nane

Mocef Marzouki (17).jpeg Moncef Marzouki

Sat, 24 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya mjini Tunis imemhukumu Rais wa zamani wa Tunisia, Moncef Marzouki kifungo cha miaka nane jela baada ya kupatikana na hatia kwa kutaka kuchochea fujo, DW imeripoti.

Marzouki ambaye alikuwa Mkuu wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia baada ya vuguvugu la mapinduzi katika Nchi za kiarabu la msimu wa machipuko mwaka 2011, anaishi nchini Ufaransa na hakuwepo Mahakamani wakati hukumu hii inatolewa.

Msemaji wa Mahakama amesema hukumu hiyo imetolewa kuzingatia kauli zilizotolewa na Marzouki zinazojumuisha uchochezi katika hotuba aliyoitoa akiwa Paris.

Mwaka 2021 Marzouki alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa kutishia usalama wa taifa baada ya kuitaka Ufaransa isitishe msaada wake kwa Rais wa Tunisia Kais Saied kwenye maandamano ya mjini Paris.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live