Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Mpya wa Malawi, Amuondolea Mstaafu Mutharika Kinga ya Kutoshtakiwa

CHAKWER.png Rais Mpya wa Malawi, Amuondolea Mstaafu Mutharika Kinga ya Kutoshtakiwa

Tue, 30 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni chini ya saa 24 tangu kuapishwa kwake, Rais mpya wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera amemuondolea kinga ya kutoshtakiwa aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Peter Mutharika ili aweze kushtakiwa, umeripoti mtandao wa Zambian Eye.

Vilevile, ili kuhakikisha kuwa mizizi ya utawala katili uliojawa na rushwa uliopita inang’olewa na kuondoka kabisa serikalini, Rais Chakwera amemtimua kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini huko Duncan Mwapasa na kumteua Inspekta Jenerali Dkt. George Kainja kuchukua nafasi hiyo.

Rais Peter Mutharika hakupata muda wa kufuta baraza lake la mawaziri ingawa alitakiwa kufanya hivyo siku chache kabla ya uchaguzi kama ambavyo katiba ya Malawi inamtaka kufanya. Mawaziri waliokuwa katika baraza lake wametakiwa kurudisha mali zote za serikali wanazozishikilia ikiwamo magari waliyopewa na serikali kufikia siku ya kesho kabla ya saa tano asubuhi.

Vilevile, kipaumbele cha kwanza cha Rais Chakwera kinatajwa kuwa uwajibikaji na kufuatilia kushitakiwa kwa wezi na mafisadi wote kama ambavyo aliahidi katika ilani ya chama chake cha Congress huku akijinadi kwa kauli ya ‘’Malawi Mpya’’, kuleta tumaini, uadilifu na kukabiliana na rushwa na ufisadi.

Wakati huohuo, kutakuwapo na mabadiliko makubwa katika Mamlaka ya Mapato ya Malawi yanayotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais Dkt. Chilima ikiwa ni juhudi za kukabiliana na rushwa katika ofisi kubwa za serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live