Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Macky Sall wa Senegal avunja serikali yake

Senegal Rais Rais Macky Sall wa Senegal avunja serikali yake

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Macky Sall wa Senegal amesaini dikrii ya kuivunja serikali yake, miezi michache kabla ya kumalizika hatamu yake ya uongozi.

Hayo yalitangazwa jana Ijumaa na Oumar Samba Ba, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Senegal ambaye ameeleza kuwa, Sall ametengua serikali yake na kuwafuta kazi mawaziri na maafisa wote wa serikali yake.

Taarifa ya Samba Ba imeeleza kuwa, Rais Sall ameunda serikali mpya chini ya Waziri Mkuu wa sasa Amadou Ba, na kwamba majina ya mawaziri hao yatangazwa karibuni.

Ifahamike kuwa, Waziri Mkuu wa sasa wa Senegal Amadou Ba ndiye mgombea wa muungano tawala wa Benno Bokk Yaakaar (BBY) katika uchaguzi ujao wa rais.

Julai mwaka huu, Sall alisema hatagombea muhula wa tatu wa urais katika uchaguzi mkuu ujao unaotazamiwa kufanyika mwaka ujao 2024.

Uamuzi huo wa Sall ambaye alisema muhula wake wa pili wa kuanzia 2019 ndio wa mwisho, ulitazamiwa kutuliza ghasia ambazo zimekuwa zikishuhudiwa nchini humo tokea mwaka 2021, katika hali ambayo taifa hilo kwa miaka mingi limekuwa likitazamwa kama kisiwa cha amani na demokrasia barani Afrika.

Senegal ilikumbwa na machafuko makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika miaka ya karibuni kuanzia tarehe Mosi hadi tatu mwezi Juni, baada ya Ousmane Sonko, mmoja wa viongozi watajika wa upinzani, kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela katika kesi ya kimaadili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live