Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Macky Sall agoma kugombea tena

Macky Sall Rais wa Senegal, Macky Sall.

Tue, 4 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Senegal, Macky Sall amemaliza uvumi ulioenea kwamba atawania muhula wa tatu na kuweka wazi kuwa hatogombea nafasi hiyo mwaka 2024, hatua ambayo inatajwa kusababisha kufanyika uchaguzi wa wazi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Kupitia hotuba hotuba yake iliyorushwa jana kwenye runinga Sall amesema: "Kumekuwa na uvumi na maoni tofauti kuhusu kugombea kwangu, muhula wa 2019, ulikuwa wa pili na wa mwisho, sitogombea katika uchaguzi ujao."

Sall ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2012 baada ya kumpiku aliyekuwa Rais wa wakati huo Abdoulaye Wade, amesema anafahamu uamuzi huo umewashangaza watu wengi lakini anaamini Senegal imejaa viongozi wenye uwezo kwa ajili ya maendeleo ya nchi hiyo.

Upinzani nchini humo ulikuwa umedhamiria kuitisha maandamano mapya iwapo kiongozi huyo angeamua kugombea tena jambo ambalo wataalamu wengi wa sheria wamesema lingekiuka katiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live