Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Lungu akubali kushindwa

C1b84ed0180bfcad424909050b95bb27 Rais Lungu akubali kushindwa

Mon, 16 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa Zambia Edgar Lungu amemkubali rasmi kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema kama mshindi wa kiti cha Urais katika uchaguzi wa Alhamis iliyopita nchini humo.

Taarifa yake inaondoa wasiwasi kwamba angepinga matokeo hayo. Lungu alisema "Kulingana na takwimu zilizotolewa katika matokeo ya mwisho, natii masharti ya kikatiba ya mabadiliko ya utawala kwa amani.

"Kwa hivyo ningependa kumpongeza kaka yangu, Rais mteule, Mheshimiwa Hakainde Hichilema, kwa kuwa Rais wa saba wa Jamhuri."

Tume ya uchaguzi ilisema Hichilema alipata kura 2,810,777 dhidi ya 1,814,201 ya Lungu, kwa maeneo yote isipokuwa moja kati ya 156 yaliyohesabiwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz