Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Kiir awapandisha vyeo wanajeshi 3,000

95e3801e75712c49c4f43b173cb57497.jpeg Rais Kiir awapandisha vyeo wanajeshi 3,000

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Salva Kiir amewapandisha vyeo wanajeshi zaidi ya 3,000 ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.

Msemaji wa Polisi, Meja Jenerali Daniel Boulo alisema mwishoni mwa wiki kuwa, Rais Kiir amewapandisha vyeo maofisa 22 wa polisi kutoka cheo cha Brigedia Jenerali kuwa Meja Jenerali, huku wengine wakipandishwa kutoka cheo cha Kanali kuwa Brigedia na Brigedia Jenerali.

Alisema maofisa waliopandishwa vyeo wanatoka katika majimbo 10 yaliyoanzishwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kuwa kwenye orodha ya kusubiri kupandishwa vyeo tangu mwaka 2017.

“Tunatakiwa kuwapandisha vyeo wafanyakazi wetu kila mwaka. Pendekezo la kuwapandisha vyeo hawa lilitolewa mwaka 2017 na 2018."

“Kuna kamati iliundwa kwa ajili ya kusimamia jambo hili na majimbo yote yalitakiwa kutoa ripoti kuhusu wafanyakazi na kuwasilisha kwa kamati hiyo pamoja na mapendekezo kwa viongozi wa jeshi na baadaye kwenda kwa Rais ambaye amewapandishwa vyeo walitangazwa,” alisema Jenerali Justin.

Chanzo: www.habarileo.co.tz