Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Kiir atangaza  wabunge wapya 550

C8988e90d8a654e88c592d78e1a0e968.jpeg Rais Kiir atangaza  wabunge wapya 550

Tue, 18 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Salva Kiir ametangaza wabunge wapya 550 ikiwa ni sehemu ya kuundwa kwa Bunge la mpito kama ilivyo katika makubaliano ya mkataba wa amani wa mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa juzi na ofisi ya Rais kwa vyombo vya habari vya serikali, ilisema Rais Kiir ameteua wabunge 550 kutoka vyama vyote vya siasa waliotia saini mkataba mpya wa amani.

Uteuzi huo umekuja siku mbili baada ya kuvunja Bunge la Kitaifa na Mabaraza ya Majimbo.

Kwa kuzingatia makubaliano ya amani, Bunge la Taifa na Mabaraza ya Majimbo yataundwa upya na kujumuisha wateuliwa wapya kutoka vyama mbalimbali.

Mkataba huo unasema kuwa Bunge la Taifa litapanuliwa kutoka wabunge 400 hadi 550 wakiwemo wawakilishi kutoka vyama vya amani, ambapo serikali ya mpito itateua wabunge 332, chama cha SPLM-IO wabunge 128, na Muungano wa Upinzani wa Sudan Kusini, 50, vyama vingine vya kisiasa vitakuwa na wawakilishi 30, wakati wafungwa wa zamani watateua washiriki 10.

Makubaliano ya amani pia yanasema kwamba, Mabaraz ya Majimbo nayo yatapanuliwa kutoka kwa wanachama 50 hadi 100, lalakini, hata hivyo, Rais, katika taarifa yake hakutangaza kupanua wala kuunda upya.

Kwa uteuuzi huo wa Rais Kiir, sasa kutakuwa na wabunge 550 na wengi ni kutoka chama chake kinachotawala cha SPLM, wakifuatiwa na chama cha upinzani cha SPLM-10 kilicho chini ya Makamu wa Rais, Riek Machar

Wajumbe wengine walioteuliwa walikuwa kutoka kwa Muungano wa Upinzani wa Sudan Kusini, Wafungwa wa Kisiasa wa Zamani, Ajenda ya Kitaifa, na Chama cha Democratic Change.

Miongoni mwa kazi kubwa zinazosubiriwa ni kuunganishwa kwa vikosi katika jeshi moja la kitaifa la kitaalam, kazi iliyoainishwa katika Sura ya II ya makubaliano ya amani ya 2018.

Chanzo: www.habarileo.co.tz