Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Kiir aamuru ulinzi barabara kuu za kiuchumi

0a9ea15af2cc87ef513de339b261ec36.jpeg Rais Kiir aamuru ulinzi barabara kuu za kiuchumi

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itamaliza kabisa changamoto za usalama barabarani hususani mashambulizi na utekaji unaofanywa na vikundi vya waasi wanaojificha misituni katika Jimbo la Ikweta ya Kati kwa kuweka ulinzi mkali wa jeshi katika barabara zote kuu za kiuchumi.

Rais Salva Kiir ameliagiza jeshi kuweka ulinzi wa saa 24 katika barabara kuu za kiuchumi na zinazotumiwa kwa wingi na wananchi ili kuruhusu shughuli zifanyike bila usumbufu wowote.

Hayo yalisemwa na Gavana wa Ikweta ya Kati, Emmanuel Adil Anthony baada ya kumaliza kikao na Rais Kiir kalichofanyika Ikulu mjini Juba.

Alisema katika mazungumzo yao, Rais Kiir alimthibitishia kuwa usalama wa barabara hizo utaimarishwa kwa gharama yoyote kwa sababu zinatengeneza uchumi wa nchi.

Maagizo hayo ya Rais Kiir yamekuja siku chache baada ya madereva nane kutoka Uganda na Kenya kuuawa katika mashambulizi ya kushtukiza yanayoaminika kufanywa na kikundi cha waasi cha NAS, Machi mwaka huu.

“Ni jambo zuri sana kwa Rais Kiir kukubali kuongeza ulinzi katika barabara zetu kuu kuondoa vitisho vyote vya usalama hali itakayoruhusu biashara kuendelea na shughuli za kibinadamu katika jimbo zima na taifa kwa ujumla,” alisema Adil.

Alisema kutokana na changamoto za kiusalama katika eneo la mpaka, alitumwa na Rais Kiir kuzungumza na vyombo vya usalama vya Uganda na baada ya kurudi alimwelezea yale waliyokubaliwa katika kikao hicho, ingawa hakuyataja.

Chanzo: www.habarileo.co.tz