Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Kiir: Tutaimarisha mapambano dhidi ya njaa

72306b1afcbdaf79f537ae97c650d3bc Rais Kiir: Tutaimarisha mapambano dhidi ya njaa

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itatoa kipaumbele katika mapambano dhidi ya njaa. Alisema hayo wakati akizungumza na wananchi akiwa kwenye ziara yake katika mji mkuu wa jimbo la Jonglei, Bor.

Kwa mujibu wa taasisi za misaada, hali inazidi kuwa mbaya nchini kwa takribani watu milioni saba sawa na asilimia 60 ya watu wanahangaika kutafuta chakula cha kutosha kila siku.

Rais Kiir pia alikagua ujenzi unaoendelea wa mradi wa barabara kuu ya Juba-Bor na kupongeza maendeleo yake yaliyofikiwa hadi sasa. Mshauri Mwandamizi wa Rais, Kuol Manyang Juuk alisema Rais Kiir ameahidi kutoa huduma kwa watu na kuwataka wananchi wasisikilize wanaharakati wanaokusudia kuigawa nchi.

Gavana wa Jimbo la Jonglei, Denay Jok Chagor alimueleza Rais Kiir kuwa raia wa jimbo hilo wanaunga mkono kikamilifu Serikali ya Mpito ya Umoja wa Kitaifa (TGoNU).

Serikali ya mseto iliundwa Februari mwaka jana kati ya Rais Kiir na kiongozi wa upinzani Riek Machar kutekeleza makubaliano ya amani.

Chanzo: www.habarileo.co.tz